SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM. Wapendwa
Katika Bwana,
Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla.
Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu
Kristo, Amina. Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa...