KWA MAELEZO ZAIDI

TANGAZA HAPA NA PATA HABARI ZA MICHEZO, KITAIFA NA KIMATAIFA HAPA VIJANA KWANZA BLOG. WASILIANA NASI: PHONE: +255 764 251 064

KWA MAELEZO ZAIDI

TANGAZA HAPA NA PATA HABARI ZA MICHEZO, KITAIFA NA KIMATAIFA HAPA VIJANA KWANZA BLOG. WASILIANA NASI: PHONE: +255 764 251 064

KWA MAELEZO ZAIDI

TANGAZA HAPA NA PATA HABARI ZA MICHEZO, KITAIFA NA KIMATAIFA HAPA VIJANA KWANZA BLOG. WASILIANA NASI: PHONE: +255 764 251 064

KWA MAELEZO ZAIDI

TANGAZA HAPA NA PATA HABARI ZA MICHEZO, KITAIFA NA KIMATAIFA HAPA VIJANA KWANZA BLOG. WASILIANA NASI: PHONE: +255 764 251 064

KWA MAELEZO ZAIDI

TANGAZA HAPA NA PATA HABARI ZA MICHEZO, KITAIFA NA KIMATAIFA HAPA VIJANA KWANZA BLOG. WASILIANA NASI: PHONE: +255 764 251 064

Thursday, October 18, 2012

SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM.


SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM. 

Wapendwa Katika Bwana, Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla. Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina. 
Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu: Tumekuja kuwapa pole na kusimama pamoja nanyi katika uchungu mkubwa mlio nao. Machozi yenu ni machozi yetu. Machozi yetu ni machozi ya Kristo mwenyewe aliye Bwana wa kanisa linaloteswa. Jipeni moyo kwa kuwa yeye aliushinda ulimwengu (Yohana 16:33). 

Tumekuja kuonyesha majonzi yetu makubwa kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania. Huu ni msiba mkubwa, na wenye msiba ni watanzania wote, wenye dini na wasio na dini. Tumekuja kushiriki pamoja nanyi kupokea matumaini ya Tanzania mpya. 

Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa. Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini. Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo:

Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha madhehebu ya dini. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake. 

 Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga. Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. 

Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo: Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa “mfumo Kristo”, na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili. Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania. Lengo la ubishi huu ni mbegu inayoweza kuratibisha na kurasmisha mateso ya kimbari na mateso ya kanisa. Matumizi mabaya ya baadhi vyombo vya habari, vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini miongoni mwa watanzania Ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria ya matumizi ya vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile, uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na ni mateso ya kimbari, mateso kwa kanisa, na kwa wantanzania wote; wawe wengi dhidi ya wachache au wachache dhidi ya wengi. Madai yasiyo ya kawaida na ya mara kwa mara kwa serikali inayodaiwa kutokuwa na dini. Madai hayo ni kama: Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili kurahisisha na kuratibisha tofauti za watanzania. 

Tunajiuliza: Likitokea la Mbagala katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa wangapi? Madai yanayojirudiarudia kutaka balozi za nchi fulani kufungwa hapa nchini. Madai haya yanaashiria kutaka balozi za nchi fulani tu ndiyo ziwe hapa nchini. Madai na mashinikizo ya Uanzishwaji wa mahakama za kidini hapa nchini Mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo ya kitaaluma na kisheria. Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika ofisi za umma, Kuhoji na kupotosha juu ya ushirikiano wa serikali na mashirika ya dini katika utoaji wa huduma za kijamii hususan afya na elimu hapa nchini Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni “wana harakati”, tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na sheria za nchi.

 Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote, makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi. Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii. Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati wakasema “sasa basi” pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei wakristo wafikishwe hapo. 

Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto; mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini.

 Tumefikia kuhoji, watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu? Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie.

 Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza kisasi ili kumtetea Kristo. 

Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma madhabahu ya dini nyingine. Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana. 

Tunawataka wakiristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakiristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama nyoka (Mathayo 10:16).
 Daima tukumbuke kuwa,

 “KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO” 
(Waefeso 6: 12). 
               Ni sisi Maaskofu wenu kwa Neema ya Mungu

Tuesday, October 9, 2012

SINTAH VS RAYUU,SINTA AMCHANA RAYUU KWA KUTAFUTA UMAARUFU KWA KUACHIA PICHA ZAKE ZA UTUPU

Baada ya muigizaji wa filamu na video model maarufu kwa jina la Rayuu kusambaza picha mtandaoni zikionesha tattoo alizojichora kwenye maeneo mbalimbali ya mwili wake kama kiunoni, shingoni, kwenye maziwa, makalio na mapaja, watu mbalimbali wamejitokeza na kumponda.
Miongoni mwao ni mtangazaji wa kipindi cha Harusini cha DTV, Sinta aliyeamua kuitumia website yake kumpa somo mugizaji huyi aliyeigiza filamu kama The Image, Trinita Show, Sound of Death, One House na zingine.

 “Hivi mtasema mimi namuonea kuandika hivi ama?? mimi ni mtambo wa kurekebisha tabia kwakweli waigizaji wengine wanatafuta umaarufu kwa kasi sana,sasa huyu so called msanii wa
Bongo wa filamu anataka atoke,na ameshatoka sasa,una pose upigwe picha ili watu wakuone ktk mitandao ili iweje? kama sio kutaka umaarufu kunuka,” ameandika Sinta.
“Rayuu or whatever u call ya self wewe ni msichana mzuri kwanini unakimbizana na umaarufu ?waacha umaarufu ukufuate sio wewe uu kimbize ndio maana watu wanawachukulia cheap kwasababu ya matendo yenu ya kukurupuka na upungufu wa mawazo. You wanna be rihhana sio? shame on you!!!!!!!!!!!!!!!!!!”

EXCLUSIVE INTERVIEW YA CLOUDS FM/ TV CHOICE FM NA RICK ROSS DSM PAMOJA NA ALIYOYASEMA.

Kupitia AMPLIFAYA ya Clouds Fm inayokua OnAiR kuanzia jumatatu mpaka ijumaa saa moja usiku, jana October 8 2012 ilisikika sehemu ya Exclusive Interview ya rapper Rick Ross kutoka kwa Obama ambae aliperform kwenye Serengeti Fiesta 2012.

Japo alisafiri safari ndefu ya masaa 25 alikua hajui atakuja kukutana na nini ila alikua na kumbukumbu tu za utotoni kuhusu Tanzania,



 Mfano mlima Kilimanjaro na mengine ila ameenjoy na atarudi anytime.
Moja ya mambo ambayo huyafahamu, Ross alitaka kwenda kwenye mbuga za Wanyama lakini muda ulikosekana, pia anasema alifurahia kuona performance ya wasanii kadhaa wa bongo waliotangulia kuperform kabla yake japo alikua haelewi.

Kuhusu jina la album yake mpya ya God forgives, I don’t yani Mungu anasemehe, mimi sisamehe , namkariri Rozay akisema.


 “kwa mtu ambae ananielewa tangu utotoni, na anaejua niliyoyapitia maishani anajua vizuri kabisa kwamba Rick Ross namjua Mungu na kumuamini, ila kuna vitu huwa vinafanyika maishani na huwa haviko mikononi mwako tena, nilitaka kuifanya hii album kama Cinema, maisha ya kila siku na nadhani niliitendea haki, nilitaka iwe stori midomoni mwa watu”